Tuesday, October 14, 2014

VIINGILIO MECHI YA SIMBA NA YANGA VYATAJWA

Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania{TFF},Boniphace Wambura akizungumza na  wanahabari wakati akitangaza viingilio na utaratibu wa kuingia uwanjani katika mechi ya watani wa Jadi kati ya Simba na Yanga unaotarajiwa kuchezwa Oct 18,2014 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam{Picha Na Othman Michuzi}
Kiingilio cha chini katika mechi ya Ligii kuu ya vodacom{VPL}Kati ya Simba na Yangaitakayochezwa Jumamosi Oct 18,2014,uwanja wa Taifa Dar es salaam ni 7,000.
Washabaiki watakaolipa kiingilio hiko ni wale watakao kaa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo jumla yake ni 36,693 katika uwanja huo wenye viti 57,558.Viingilio vingine ni 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa,20,000 kwa VIP B na C wakati A itakuwa 30,000.
Tiketi zitakazotumika katika mechi hiyo ni za elektroniki na zimeanza kuuzwa jana Oct 13,2014.Tiketi zinapatikana kwa mtandao wa M-PESA,CRDB Simbanking na maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayoyapo zaidi ya mia moja sehemu mbali mbali ya jiji la Dar es salaam.

Mechi hiyo namba 27 itachezeshwa na mwamuzi Israel Mjuni Nkongo akisaidiwa na John Kanyenye na Ferdinad Chacha itaanza saa kumi kamili jioni.Kamishna wa mechi hiyo ni Salum Kikwamba akitokea Mkoani Kilimanjaro.
Mashabiki wanatakiwa kununua tiketi hizo mapema kwani hazitauzwa uwanjani siku ya mechi.Milango yote ukiwamo ule wa upande wa Mbagala{uwanja wa ndani}itafunuliwaitafunguliwa kwaajili ya washabiki na itakuwa wazi kuanzia saa 4 asubuhi.

Magari maalum yenye stika tu ndio yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani kwa kupitia barabara ya Mandela.Pia washabiki hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa na silaha,vitu vya chuma na mabegi makubwa.Barabara ya kuingilia upande wa Chang'ombe itafungwa kwa watumiaji wa magari.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA{TFF}

No comments:

Post a Comment