Tuesday, October 14, 2014

NI MIAKA KUMI NA TANO SASA TANGU ALIPOTUTOKA BABA WA TAIFA HILI AU MUASISI WA TAIFA HILI..MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE WENGI WALIPENDA KUMUITA MZEE KIFIMBO CHEZA KUTOKANA NA NA KUPENDA KUTEMBEA NA KIFIMBO CHAKE...KIUKWELI ALIKUWA KIONGOZI MWENYE MAPENZI YA DHAATI NA TAIFA LAKE,HAKUWA MWENYE TAMAA,WALA MAJIVUNO...HEBU TAZAMA TASWIRA ZAKE MBALI MBALI ENZI HIZO ALIPOKUWA KIONGOZI..
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akisalimiana na Rais wa Uganda Wakati huo Iddi Amini Dadah wakati wa kikao cha OAU mjini Addis Ababa,Ethiopia enzi hizo.Kushoto kwa Mwalimu ni Waziri wa Mambo ya Nje Mhe John S amweli Malecela
Mwalimu akimkumbatia Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kutoa hotuba ya kukubali matokeo ya Urais alipogombea kwa mara ya kwanza mwaka 2005. Mhe Benjamin Mkapa alishinda
 Mwalimu akiwa na mume wa Malkia wa Uingereza, Prince Philip

VIINGILIO MECHI YA SIMBA NA YANGA VYATAJWA

Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania{TFF},Boniphace Wambura akizungumza na  wanahabari wakati akitangaza viingilio na utaratibu wa kuingia uwanjani katika mechi ya watani wa Jadi kati ya Simba na Yanga unaotarajiwa kuchezwa Oct 18,2014 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam{Picha Na Othman Michuzi}
Kiingilio cha chini katika mechi ya Ligii kuu ya vodacom{VPL}Kati ya Simba na Yangaitakayochezwa Jumamosi Oct 18,2014,uwanja wa Taifa Dar es salaam ni 7,000.
Washabaiki watakaolipa kiingilio hiko ni wale watakao kaa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo jumla yake ni 36,693 katika uwanja huo wenye viti 57,558.Viingilio vingine ni 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa,20,000 kwa VIP B na C wakati A itakuwa 30,000.
Tiketi zitakazotumika katika mechi hiyo ni za elektroniki na zimeanza kuuzwa jana Oct 13,2014.Tiketi zinapatikana kwa mtandao wa M-PESA,CRDB Simbanking na maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayoyapo zaidi ya mia moja sehemu mbali mbali ya jiji la Dar es salaam.

Mechi hiyo namba 27 itachezeshwa na mwamuzi Israel Mjuni Nkongo akisaidiwa na John Kanyenye na Ferdinad Chacha itaanza saa kumi kamili jioni.Kamishna wa mechi hiyo ni Salum Kikwamba akitokea Mkoani Kilimanjaro.
Mashabiki wanatakiwa kununua tiketi hizo mapema kwani hazitauzwa uwanjani siku ya mechi.Milango yote ukiwamo ule wa upande wa Mbagala{uwanja wa ndani}itafunuliwaitafunguliwa kwaajili ya washabiki na itakuwa wazi kuanzia saa 4 asubuhi.

Magari maalum yenye stika tu ndio yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani kwa kupitia barabara ya Mandela.Pia washabiki hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa na silaha,vitu vya chuma na mabegi makubwa.Barabara ya kuingilia upande wa Chang'ombe itafungwa kwa watumiaji wa magari.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA{TFF}


BURIANI BURIANI BURIANI PROFESA ALI MAZRUI

 Oktoba 14,mwaka jana Uwakilishi wa Kudumu Wa Jamhuri Y a Muungano W a Tanzania katika Umoja Wa Mataifa uliandaa hafla ya kwanza ya aina yake ya kumkumbuka na kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Hafla iliyoudhuriwa na wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi zao hapa Umoja Wa Mataifa na Wageni Mbalimbali.
Ni hafla iliyoambatana na uzinduzi wa kitabu kinachomuhusu Baba wa Taifa.Kitabu hicho kiliandikwa kwa ufundi mkubwa na Profesa Ali Mazrui kwa kushirikiana na Profesa Linda Mhando ambaye ni Mtanzania.
Uwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa umepokea kwa masikitiko makubwa  taarifa za kufariki Profesa Ali Mazrui.Ulitufunza meengi siku ile kuhusu Mwalimu na ambayo mengine hayajawahi kuandikwa popote.
Mwenyezi mungu aiweke roho ya marehemu Profesa Ali Mazrui mahala pema peponi
AMEN.

MAKAMU WA RAIS DKT  BILAL AWAONGOZA WATANZANIA NA WANANCHI WA SENGEREMA KUMZIKA DKT SHIJA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Mohamed Gharib Bilal,akitoa heshima zake za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola,Marehemu Dkt William Shija,wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika kijijini kwake,Nyampande Wilaya ya Sengerema Mkoa Wa Mwanza,jana Oct 13 2014.
Spika wa Bunge la Jamhuri,Mhe.Anne Makinda,akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mabunge ya Nchi Wanachama  wA Jumuiya ya Madola,marehemu Dkt William Shija,wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika Kijijini kwake Nyampande Wilaya ya Sengerema,Mkoa Mwanza jana Oct 13 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Mohamed Gharib Bilalakiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mabunge ya Nchi Wanachama Wa Jumuiya ya Madola,Marehemu Dkt William Shija wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika kijijini kwake Nyampande Wilaya  Sengerema,Mkoa Mwanza,jana Oct 13 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Mohamed Gharib Bilal akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mabunge ya Nchi Wanachama Wa Jumuiya ya Madola,Marehemu Dkt William Shija wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika Kijijini kwake Nyampande Wilaya Sengerema,Mkoa Mwanza,jana Oct 13 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania,Dkt Mohamed Gharib Bilal akitia saini katika kitabu cha maombelezi wa msiba wa aliyekuwa Katibu Mkuu Wa Chama Cha Mabunge wa Jm Nchi Wanachama Wa Jumuiya Madola,marehemu,Dkt William Shija wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika kijijini kwa marehemu Nyampande Wilaya Sengerema Mkoa MWANZA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano,Dkt Bilal akiwafariji familia ya aliyekuwa Katibu Mkuu Wa Mabunge Ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola,Marehemu Dkt William Shija wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika kijijini kwakwe Nyampande Wilaya Sengerema,Mkoa Mwanza jana Oct 13 2014.

ZOEZI LA UOKOAJI MIILI KATIKA AJALI YA MITUMBWI KATIKA ZIWA TANGANYIKA LASITISHWA

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akiongea na waandishi wa habari{ ambao hawapo pichani}ofisini kwake juu ya kusitisha zoezi la uopoaji wa miili ya ajali ya mitumbwi iliyotokea hivi karibuni katika kijiji cha Kalalangabo ziwa Tanganyika.
Na Editha Karlo wa Blog ya Jamii,Kigoma.

Serikali ya mkoa wa Kigoma imesitisha uopoaji wa miili ya ajali ya mitumbwi miwili ya maharusi iliyotokea hivi karibuni katika Ziwa Tanganyika kwenye kijiji cha Kalalangabomwambao mwa ziwa Tanganyika.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kanali Mstaafu Issa Machibya alisema vikosi mbali mbali vya uokoaji kwa kushirikiana na jeshi la wananchi{JWTZ}wakishirikiana  na wananchi wamefanya kazi kubwa  sana ya kuopoa miili kwa kipindi cha siku tatu mfululizo.

Alisema jumla ya miili kumi ilipatikana katika zoezi hilo la uokoaji lakini hivi sasa wameiachia uongozi wa serikali ya kijiji ya Kalalangabo kuendelea kutoa taarifa kama kuna miiili mingine itaendelea kuibuka.

"Ile mitumbwi ilikuwa imejaza sana watu ambayo idadi yake mpaka sasa bado haijajulikana kwani walivyokuwa wanaenda kupanda walikuwa na hiace tatu,pikipiki kumi na vyote vilikuwa na ndugu,jamaa na wapambe wa maharusi.

Ilikuwa mitumbwi miwili ya kienyeji tena ile inayotumika kuvulia samaki na dagaa,sasa tunahofia kwamba miili mingi itakuwa bado ipo majini kwani jana waokoaji walifanikiwa kupata baadhi ya vitu majini kama vile simu,nguo na saa"Alisema Machibya.

Mkuu wa mkoa aliwataka wananchi kuacha kutumia vyombo visivyo rasmi katika rasmi na ambavyo havijasajiriwa na mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini{SUMATRA}Pia aliwataka wavuvi na wale wenye vyombomajini waache tabia ya kusafirisha abiria kwa kutumia mitumbwi ya kuvulia dagaa ili kuepuka ajali.

"Kuna siku mimi na kamati yangu ya ulinzi na usalama tutaingia majini wenyewe siku nzima kufanya ziara ya ghafla na kuwakamata wale wootewanaokiuka sheria za kusafirisha abiria ziwani"alisema Machibya.

Machibya alisema wamiliki wa vyombo hivyo bado hawajafahamika hivyovyombo vya usalama bado vinaendelea na juhudi za kuwatafuta wamiliki wa mitumbwi hiyo ili waweze kufikishwa katika sheria.
Hii ndio mitumbwi iliyopigwa na wimbi kuzama na kusababisha maafa,ilikuwa imebeba maharusi na ndugu na jamaa na wapambe,watu wanaokadiriwa zaidi ya 80 wanakadiriwa walikuwemo katika mitumbwi hii wakisindikiza maharusi.

RAIS KIKWETE ATOA HOTUBA KATIKA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE MKOANI TABORA

Rais wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi wa mkoa wa Tabora katika kilele cha mbio za mwenge 2014 zilizofanyika katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mjini Tabora Leo{Picha na Fredy Maro}


NEWS ALERT:LORI LA MAFUTA LAWAKA MOTO MBAGALA JIJINI DAR USIKU WA KUAMKIA LEO


Awali,lori hilo pamoja na kupiga mwereka halikufanya madhara yeyote wala dalili ya kusema litawaka moto.Ila baada ya muda likaja kundi la vijana likiwa na madumu pamoja na mifuko ya plastiki na kuanza kuchukua mafuta yalimo katika lori hilo hali iliyopelekea kutokea mlipuko mkubwa ulioteketeza kabisa lori hilo.

Haijafahamika mpaka sasa kama kuna mtu yeyote amepoteza maisha katika moto huo,ila hasara kubwa imeonekana kwa nyumba tatu zilizokuwa jirani na eneo hilo la tukio ambazo zimeteketea kabisa na moto huo.Nyumba moja ni ya makaazi ya watu,ingine ni duka la jumla la mchele pamoja na nyumba ya kulala wageni,kiwinga85.blogspot.com inaendelea kufatilia kwa ukaribu tukio hilo na tutaendelea kujuzana.
Sehemu ya lori likiwa limeteketea kabisa.
Sehemu ya wakaazi wa maeneo hayo wakiangalia kilichotokea huku wakiwa hawaamini wanachokiona.
Sehemu ya nyumba zilizoteketea kwa mtot huo.