Tuesday, October 14, 2014

ZOEZI LA UOKOAJI MIILI KATIKA AJALI YA MITUMBWI KATIKA ZIWA TANGANYIKA LASITISHWA

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akiongea na waandishi wa habari{ ambao hawapo pichani}ofisini kwake juu ya kusitisha zoezi la uopoaji wa miili ya ajali ya mitumbwi iliyotokea hivi karibuni katika kijiji cha Kalalangabo ziwa Tanganyika.
Na Editha Karlo wa Blog ya Jamii,Kigoma.

Serikali ya mkoa wa Kigoma imesitisha uopoaji wa miili ya ajali ya mitumbwi miwili ya maharusi iliyotokea hivi karibuni katika Ziwa Tanganyika kwenye kijiji cha Kalalangabomwambao mwa ziwa Tanganyika.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kanali Mstaafu Issa Machibya alisema vikosi mbali mbali vya uokoaji kwa kushirikiana na jeshi la wananchi{JWTZ}wakishirikiana  na wananchi wamefanya kazi kubwa  sana ya kuopoa miili kwa kipindi cha siku tatu mfululizo.

Alisema jumla ya miili kumi ilipatikana katika zoezi hilo la uokoaji lakini hivi sasa wameiachia uongozi wa serikali ya kijiji ya Kalalangabo kuendelea kutoa taarifa kama kuna miiili mingine itaendelea kuibuka.

"Ile mitumbwi ilikuwa imejaza sana watu ambayo idadi yake mpaka sasa bado haijajulikana kwani walivyokuwa wanaenda kupanda walikuwa na hiace tatu,pikipiki kumi na vyote vilikuwa na ndugu,jamaa na wapambe wa maharusi.

Ilikuwa mitumbwi miwili ya kienyeji tena ile inayotumika kuvulia samaki na dagaa,sasa tunahofia kwamba miili mingi itakuwa bado ipo majini kwani jana waokoaji walifanikiwa kupata baadhi ya vitu majini kama vile simu,nguo na saa"Alisema Machibya.

Mkuu wa mkoa aliwataka wananchi kuacha kutumia vyombo visivyo rasmi katika rasmi na ambavyo havijasajiriwa na mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini{SUMATRA}Pia aliwataka wavuvi na wale wenye vyombomajini waache tabia ya kusafirisha abiria kwa kutumia mitumbwi ya kuvulia dagaa ili kuepuka ajali.

"Kuna siku mimi na kamati yangu ya ulinzi na usalama tutaingia majini wenyewe siku nzima kufanya ziara ya ghafla na kuwakamata wale wootewanaokiuka sheria za kusafirisha abiria ziwani"alisema Machibya.

Machibya alisema wamiliki wa vyombo hivyo bado hawajafahamika hivyovyombo vya usalama bado vinaendelea na juhudi za kuwatafuta wamiliki wa mitumbwi hiyo ili waweze kufikishwa katika sheria.
Hii ndio mitumbwi iliyopigwa na wimbi kuzama na kusababisha maafa,ilikuwa imebeba maharusi na ndugu na jamaa na wapambe,watu wanaokadiriwa zaidi ya 80 wanakadiriwa walikuwemo katika mitumbwi hii wakisindikiza maharusi.

No comments:

Post a Comment