Monday, January 23, 2012

BREAAKING NEWZ...BREAKING NEWZ...BREAKING NEWZ..!!
BREAKING NEWZ...BREAKING NEWZ...BREAKING NEWZ..!!

                                                              MADAKTARI WAAMUA KUGOMA RASMINI KUANZIA LEO


Lile sakata la Madaktari na Serikali limefikia mahala si pazuri baada ya Madktari hao kuamua kuanza kugoma siku ya leo tarehe 24/january/2012.


Uamuzi huu umetolewa jana katika mfululizo wa mikutano waliyoianza toka hapo jumatano ya wiki iliyopita(18/januari/2012)katika kujaribu kutafuta suluhu ya matatizo yao katika sekta ya Afya kwa ujumla,Juhudi hizo hazikuzaa matunda kutoka kwa Serikali kuanzia Wizara ya Afya mpaka ofisi ya Waziri Mkuu ambapo nako kutozaa matunda.


Madaktari/Watumishi wa Afya hao wanamadai kadhaa kama:-


*Kuboresha huduma za Afya nchini(Hospitali na vitanda kwa kila mgonjwa wa afya inawezekana.


*Maslahi duni kwa watumishi wa sekta ya afya.


*Malipo kwa kazi za ziada kwani Madaktari wanalipwa Tsh 10,000/= kwa kukesha na kufanya kazi kwa masaa 36 tofauti na taratibu za serikali kwani ilitakiwa wawe wanalipwa Tsh40,000/=(half pediem)kama taratibu za serikali zinavyoonyesha lakini viongozi wa Wizara hasa Mama Blandina Nyoni ndio wanaokwamisha.


*Haki ya kupewa nyumba ama posho ya nyumba kama muongozo wa utumishi wa umma wa serikali ya Tanzania ule wa mwaka 1994 na wa mwaka 2009 unavyopendekeza.


*Kulipwa posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi(Risk Allowance).


*Kuondolewa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Bi Blandina Nyoni anayeonekana ni kikwazo katika juhudi za msingi za kuboresha sekta ya Afya Nchini.


Bi Blandina Nyoni anatuhumiwa kutoa kauli ya kejeli kwa watumishi wa afya kuwa anamshukuru baba yake kwa kumkataza kusomea mambo ya afya kwani sekta ya afya haifai na ndio maana licha ya kufaulu masomo ya sayansi baba yake alimshauri asomee uhasibu.

Maamuzi hayo magumu toka kwa Madaktari/Watumishi hao wa afya yalifikiwa jana katika mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa DON BOSCO UPANGA ikiwa ni muendelezo wa mikutano yao isiyokoma toka hapo ilipoanza jumatano iliyopita.

No comments:

Post a Comment