Tuesday, October 14, 2014

NEWS ALERT:LORI LA MAFUTA LAWAKA MOTO MBAGALA JIJINI DAR USIKU WA KUAMKIA LEO

Sehemu ya mabaki ya lori lilitoketea kwa moto usiku wa kuamkia leo maeneo ya Mbagala,Jijini Dar es salaam,Baada ya kupiga mueleka likiwa katika hati hati ya kulikwepa gari lingine lililokuwa linatokea Kongowe ambalo liliingia ghafla barabarani bila tahadhari.

Awali lori hilo baada ya kupiga mweleka halikufanya madhara yeyote wala kuonyesha dalili kama litawaka moto.Ila baaada ya muda likaja kundi la vijana likiwa na madumu na mifuko ya plastiki na kuanza kuchukua mafuta yaliyokuwemo katika lori hilo hali iliyopelekea kutokea mlipuko mkubwa ulioliteketeza kabisa lori hilo.

Haijafahamika mpaka sasa kama kuna mtu yeyote aliyepoteza maisha kutokana na moto huo,Ila hasara kubwa imeonekana kutokea kwa nyumba tatu zilizokuwa jirani na eneo la tukio ambazo zimeteketea kwa moto huo,Nyumba moja ni ya makaazi ya watu,ingine ni duka la jumla la mchele pamoja na nyumba ya kulala wageni...kiwinga85.blogspot inaendelea kufatilia kwa ukaribu tukio hilo na tutaendelea kujuzana.

Sehemu ya lori hilo likiwa limeteketea kabisa.

Sehemu ya baaadhi ya wakaazi maeneo hayo wakiangalia kilichotokea huku wakiwa hawaamini wanachokiona.

Sehemu ya nyumba zilizoteketea kwa moto.

No comments:

Post a Comment