Tuesday, October 14, 2014

AJALI YAUA WAWILI NA KUJERUHI WENGINE WAWILI MKOANI LINDI

Watu wawili wamekufa na wengine wawili kujeruhiwa baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Michenga,Wilaya ya Ruangwa Ruangwa Mkoani Lindi. Kamanda wa polisi Mkoa wa Lindi ACP Renatha Mzinga alisema gari hoiyo aina ya Toyota Rav4 yenye namba za usajili T574 CWC iliyokuwa inaendeshwa na Mohamed Mchalanganya {27} iliacha njia na kupinduka  katika barabara ya Ruangwa-Nanganga,ilitokea jana saa 11.30 jioni.

Kamanda Mzinga aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Binasa Mapua 
{51} mkazi wa Tabata-Dar-es-salaam na Elizabeth Chipoleka {53} mkazi wa Yombo,Dar es salaam.

Kamanda Mzinga amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Mussa Mchalanganya na Rashid Mchalanganya ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha usafirishaji {NIT},ambapo wote ni wakaazi wa Tabata 
,Dar es salaam.Dereva wa gari hilo ametiwa mbaroni na upelelezi bado unaendelea kujua chanzo hasa cha ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment